Wakenya Tafakari Wasia Wa Papa Francis

Wakenya Tafakari Wasia Wa Papa Francis

by -
0 506
Papa Francis akiwapungia mkono wakenya waliotamani kumsalimia mjini Nairobi.

Wakenya sasa wamesalia kutafakari wasia uliotolewa na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis aliyezuru Kenya kwa siku tatu na kuondoka Ijumaa iliyopita.

Kiongozi huyo atakumbukwa kwa miaka mingi jinsi alivyoshauri serikali kuwajali maskini na watu wasio na makao, huku akionesha moyo wa dhadi alipokongamana na maelfu ya vijana katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Wasia wake kabla ya kuondoka kuelekea Uganda ulikuwa kukemea ufisadi na ukabili, akisema ulafu una adhabu ya mauti.

Papa mtakatifu alitahadharisha kuhusu chuki inayoendelezwa kote duniani kwa kutumia dini.

Akizungumza alipokutana na viongozi wa kidini katika ubalozi wa Vatican jijini Nairobi Papa alisisitiza umuhimu wa kuwafunza
vijana kujitenga na chuki inayoendelezwa kwa kutumia jina la Mungu akisema ni kinyume cha mapenzi ya mwenyezi Mungu.

Papa alieleza haja ya kukomesha chuki ya kidini kote duniani ikiwa ndio sababu ya kimsingi iliyomleta barani Afrika.

Alidokeza hayo wakati kukiwa na misururu ya mashambulio yanayofungamishwa na dini, huku akikashifu mafunzo ya itikadi kali.

Katika ziara ya papa nchini Kenya maafisa wa usalama zaidi ya 10,000 walipiga doria hasa katika jiji la Nairobi.

Papa alisisitiza kuwa ufisadi unaweza kungamiza taifa lolote, akitoa mfano wa sukari ambayo huwa tamu lakini husababisha ugonjwa wa kisukari.

Alikariri kuwa ufisadi huwanyima watu raha na amani pia husababisha maafa, akiongeza kuwa hata katika makao ya Vatican mjini Roma kuna kasumba ya ufisadi.

Alikariri umuhimu wa elimu, nafasi za kazi na kukabili umaskini, akiitaja kama mikakati ambayo italeta matumaii kwa mamillioni ya vijana kote dunaini.

Comments

comments