Shule ya wasichana ya Voi yafungwa kwa muda

Shule ya wasichana ya Voi yafungwa kwa muda

by -
0 431
Lango kuu la shule ya upili ya Voi ambayo sasa ni ya wasichana pekee

Wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Voi wamesusia masomo wakilalamikia vumbi nyingi inayotokana na ujenzi wa reli ya kisasa karibu na shule hiyo.

Wamesusia masomo wakitaka shule yao ihamishwe ili kuepuka madhara ya kiafya.

Wanafunzi hao wanasema vumbi na kelele zinazosababishwa na ujenzi wa reli hiyo vimekuwa kero kwao hivyo kuathiri masomo.

Ilibidi usimamizi kufunga shule hiyo na kutuma wanafunzi nyumbani.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi Mary Mwasaru anasema suala hilo sasa linakanganya kwa kuwa awali kulikuwa na makubaliano ya kuhamisha shule hiyo hadi sehemu nyingine ila baadhi ya viongozi wanapinga.

Bi Mwasaru ameambia Baraka Fm kuwa ni kana kwamba viongozi sehemu hiyo wameingiza siasa katika suala hilo.

“County education board ilipokaa baada ya kuona kwamba kuna sintofahamu, walitembelea maeneo yote na wakapendekeza ipelekwe pale vindo multipurpose society. MCA ameshikilia ya kwamba hiyo shule iko katika wadi yake na haiwezi kupelekwa kwa wadi nyingine” alisema Bi Mwasaru.

Mwalimu huyo mkuu sasa anasema hawawezi kufungua shule hiyo hadi Gavana wa Taita Taveta John Mrutu atakapotoa mwelekeo.

“Saa hii masomo yameshindikana maanake watoto wamesema pasipo kuambiwa tunapelekwa wapi hatuko tayari kurudi darasani. Tunangojea tupewe directions. Jibu liko kwa Gavana. Gavana akishawajibu directors vile atakavyowaeleza, tuwajulishe wanafunzi warudi.” Alisisitiza Bi Mwasaru.

Awali wanafunzi hao waliandamana hadi ofisi za serkali kupitisha kilio chaokabla ya kususia masomo.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES