Matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar wafutiliwa mbali

Matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar wafutiliwa mbali

by -
0 562
Mgombea Edward Lowassa akihutubiwa wanahabari jijini Dar es Salaam. Picha na: Joseph Jira

Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar imetangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi mkuu, katika nchi hiyo ambayo iko chini ya muungano wa Tanzania.

tume hiyo inasema wamechukua hatua hiyo kufuatia madai ya udangayifu kisiwani Zanzibar.

Tangazo hilo linakuja siku moja tu baada ya mgombea wa chama cha upinzani –CHADEMA kujitangaza mshindi, katika uchaguzi wa urais huko Zanzibar.

Hayo yakijiri mgombea urais wa chama cha upinzani Chadema nchini Tanzania Edward Lowasa amesema anapinga matokeo ya uchaguzi mkuu yanayoendelea kutangazwa nchini Tanzania kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo.

Lowassa anasema matokeo hayo yanaonyesha wazi kuwa yamebadilishwa katika baadhi ya maeneo.

Ameitaka tume ya uchaguzi nchini humo NEC kusitisha zoezi hilo na kuanza kuhesabu kura upya.

Amesema matokeo yanayotangazwa na tume ya NEC yanampendelea mgombea wa CCM John Magufuli.

Ametishia kuchukua hatua ambayo hajaitangaza iwapo tume hiyo itaendelea kutangaza matokeo.

Mwandishi wa Baraka Fm aliye Dar es Salaam Joseph Jira anasema kufikia Jumatano mchana tume hiyo ilikuwa imekwisha hesabu matokeo ya uchaguzi kutoka majimbo 162 kati ya 264.

John Magufuli aliyewania urais kupitia chama tawala CCM anaongoza katika matokeo hayo ya awali.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES