Ashtakiwa kwa madai ya kupanga njama ya kumwua mumewe.

Ashtakiwa kwa madai ya kupanga njama ya kumwua mumewe.

by -
0 574

Mahakama ya Mombasa imeipa polisi siku 10 kukamilisha uchunguzi kuhusu kesi ambapo mwanamke mmoja akishirikiana na mfanyakazi wake wa nyumbani wanadaiwa kupanga njama ya kumwua mumewe.

Hakimu Viola Yator ametoa mwelekeo huo baada ya afisa wa upelelezi katika kesi hiyo Police Constable Dominic Kiptum kuwasilisha ombi hilo.

Mahakama imeambiwa – Rose Adhiambo Raminya ambaye ni mke wa mlalamishi, pamoja na mfanyikazi wake wa nyumbani Doris Akinyi Nyaoro walipanga kumwua – Polycarp Okumu kati ya tarehe 20 na 26 mwezi oktoba eneo la Kisauni hapa Mombasa.

Inadaiwa kuwa njama ya kumuua Okumu ilitibuka,baada ya mshukiwa Adhiambo alipojaribu kutoa shilingi milioni 1.2 katika akaunti ya benki ya mumewe ili kuwalipa waliostahili kutekeleza mauaji hayo.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 9 mwezi ujao.

Comments

comments