Polisi Mombasa wasema wamemkamata mshukiwa mkuu wa ugaidi

Polisi Mombasa wasema wamemkamata mshukiwa mkuu wa ugaidi

by -
0 428
Kamishna wa Mombasa Nelson Marwa

Maafisa wa polisi hapa Mombasa wametaja oparesheni ya kumkamata mshukiwa wa ugaidi Lukeman Khatibu Mwashasha kuwa ni hatua kubwa ya kupiga vita ugaidi haswa katika kaunti ya Mombasa.

Mshukiwa huyo wa ugaidi mwenye umri wa miaka 20, alikamatwa pamoja na washukiwa wengine katika eneo la Majengo usiku wa kuamkia Alhamisi.

Kamishna wa Mombasa Nelson Marwa anasema vita dhidi ya ugaidi sasa vinaonekana kufaulu, huku akisisitiza washukiwa wengine wanaswakwa.

“As I speak now yeye ni mgeni wa serikali..ako ndani..Lukeman. anadodge anadodge anaenda kona ile anarudi hukoo ee..si ndio..saa hizi yeye ni mgeni wa serikali. Tumesema asipigwe asikuwe harassed..apewe chai vizuri arelax..he is a government guest na mwenzake..” alisema kamishna Marwa.

Mshukiwa huyo alikamatwa akiwa na Magwanda ya polisi,visu kadhaa na vifaa vingine.

Wakati huo huo polisi wamemfungulia mashtaka pamoja na mshukiwa mwingine waliokamatwa pamoja kwa jina Swaleh Mbarak.

Wameshtakiwa kwa madai ya kumshambulia kwa kisu na kumjeruhi afisa wa polisi , umiliki wa silaha hatari kinyume cha sheria pamoja na kupatikana na dawa za kulevya.

Mahakama imesema kesi dhidi yao itaendelea tarehe 2 mwezi Novemba mwaka huu.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES