Bunge la Mombasa lajadili hoja kuwaadhibu wanafunzi waliogoma na kuzua vurugu

Bunge la Mombasa lajadili hoja kuwaadhibu wanafunzi waliogoma na kuzua vurugu

by -
0 403
Lori za kaunti ya Mombasa zikichomeka kufuatia vurugu za wanafunzi: Picha na Halahala Wachu

Hoja imewasilishwa katika bunge la kaunti ya Mombasa kupendekeza adhabu kali kwa wanafunzi wa chuo cha kiufundi mjini Mombasa waliogoma Jumatatu na kuzua vurugu na pia kuharibu mali.

Hoja hiyo iliwasilishwa bungeni na mwakilishi wa wadi ya Port-reitz Fadhili Mwalimu Kutaka wanafunzi walioharibu magari ya kaunti wachukuliwe hatua.

Wabunge waliendelea kujadili hoja hiyo Jumatano mchana ambapo idadi kubwa ya wabunge walionekana kuunga mkono hoja hiyo.

Fadhili anataka hoja hiyo ipitishwe ili kuadhibu wanafunzi waliohusika kuharibu mali ya kaunti.

Alisema inapaswa kuwe na sheria itakayosaidia kudhibiti visa vya wanafunzi kuzua vurugu.

Wanafunzi hao waligoma na kuzua vurugu Jumatatu kulalamikia nyongeza ya karo, hatua iliyosababisha usimamizi wa Technical University of Mombasa kufunga chuo hicho.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES