Kamishna Nelson Marwa ataja magari yanayotumiwa kusambaza mihadarati Mombasa

Kamishna Nelson Marwa ataja magari yanayotumiwa kusambaza mihadarati Mombasa

by -
0 486

Idara ya usalama kaunti ya Mombasa imetaja hadharani baadhi ya magari inayosema yanatumiwa kulangua dawa za kulevya mjini Mombasa.

Kulingana na kamishna wa Mombasa Nelson Marwa magari hayo hutumiwa kuuza dawa hizo maeneo ya Tudor, Old Town na Majengo.

Akizungumza Jumanne mjini Mombasa katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa Marwa alimwagiza afisa mkuu wa upelelezi mjini Mombasa Henry Ondiek kufika katika ofisi za mamlaka ya mapato nchini KRA ili kubaini wamiliki wa magari hayo.

Marwa vile vile alisema magari hayo yamekuwa yakitumika kusambaza mihadarati kwa wanafunzi.

Naye gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho aliagiza idara ya polisi kuchukua hatua za haraka dhidhi ya wanaomiliki magari hayo.

“Kama kaunti kamishna ametoa magari namba, tunataka polisi mshike hayo magari na tuyaone kama yameshikwa, na hawa wenye runinga waje waone kabisa wameshikwa, wajue ni nani na hatua gani itachukuliwa ndio ikome mara moja, sio kila siku kuongea na hakuna kitu inafanyika,” Alisema gavana Joho.

Walikuwa wakizungumza katika sherehe za kutambua mashujaa waliochangia maendeleo nchini.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES