Hezron Awiti awakosoa wanasiasa Mombasa

Hezron Awiti awakosoa wanasiasa Mombasa

by -
0 385
Mbunge wa Nyali Hezron Awiti na gavana Hassan Ali Joho katika mkutano wa awali.

Mbunge wa Nyali Hezron Awiti amekosoa mashirika ya kijamii pamoja na viongozi wa kaunti ya Mombasa kwa kutojitokeza na kutetea haki za maafisa wa usalama wakati wanapouawa na magaidi.

Awiti alisema maafisa wa usalama wanahaki sawa na mwananchi wa kawaidai, japo viongozi hao husita kujitokeza na kuzungumza wakati polisi anaposhambuliwa.

Akizungumza katika sherehe za kukumbuka mashujaa mjini Mombasa siku ya jumanne, Awiti aliongeza kuwa utovu wa usalama umeathiri pakubwa sekta ya biashara ukanda wa pwani.

Vile vile alikosoa hatua ya bandari ya KPA kupunguza idadi ya wafanyakazi na badala yake akapendekeza wapewe ajira kaunti ya Lamu kunakoendelea ujenzi wa bandari mpya ya LAPSET.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES