Benki iliyovamiwa eneo la Bondeni mapema mwezi huu kuhamishwa

Benki iliyovamiwa eneo la Bondeni mapema mwezi huu kuhamishwa

by -
0 360

Polisi hapa Mombasa wanasema wanafanya mashauriano na usimamizi wa benki ya Gulf African kuhusu kuhamisha benki hiyo iliyovamiwa eneo la Bondeni mjini Mombasa yapata majuma matatu yaliyopita.

Polisi hao wameambia Baraka Fm kwamba benki hiyo huenda ikahamishiwa upande wa pili wa barabara, mkabala na sehemu iliyoko kwa sasa.

Kamanda wa polisi eneo la pwani Francis Wanjohi anasema washukiwa wa ujambazi hutumia njia za vichochoro zilizo karibu na benki hiyo kutorokea sehemu za Old Town baada ya kutekeleza uhalifu.

Katika uvamizi huo, afisa mmoja wa polisi aliuawa na bunduki yake aina ya G3 kuibwa ikiwa na risasi kadhaa.

Bunduki hiyo haijapatikana kufikia sasa.

Polisi walihusisha watu waliovamia benki hiyo na kundi la kigaidi la Alshabaab.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES