FIFA U-17: Nigeria Yaadhibu Marekani.

FIFA U-17: Nigeria Yaadhibu Marekani.

by -
0 332
Mchezaji wa Golden Eaglets ya Nigeria aking'ang'ania mpira na mpinzani wa Marekani katika mechi ya kombe la dunia kwa vijana huko Chile.

Nigeria imeanza vyema harakati za kutetea taji kandanda katika michuano ya kombe la dunia kwa vijana walio na umri chini ya miaka 17.

Katika siku ya kwanza ya kinyang’anyiro hicho mapema Jumapili Nigeria ilichapa Marekani mabao 2-0.

Michuano hiyo ya vijana chipukizi inaendelea nchini Chile huku wenyeji Chile wakitoka sare ya bao moja na Croatia katika mechi ya kufungua mashindano.

Kando na Nigeria bara la Afrika pia linawakilishwa na timu zingine tatu -Mali, Guinea na Afrika Kusini.

Mapema mwezi machi Mali ilitwaa kombe la Afrika kwa vijana wa umri usiozidi miaka 17.

Mechi ya fainali katika michuano hiyo ya kombe la dunia kwa vijana huko Chile itasakatwa Novemba tarehe 8.

Nigeria –bingwa mara 4 wa kombe hilo ilishinda makala ya mwaka 2013 katika muungano wa UAE kwa kushinda Mexico mabao 3-0 katika fainali.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES