Mshukiwa wa wizi auawa na polisi Mombasa.

Mshukiwa wa wizi auawa na polisi Mombasa.

by -
0 400

Polisi wamemwua kwa kumpiga risasi mshukiwa anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi haramu kwa jina wakalikwanza eneo la Bombolulu hapa Mombasa.

Polisi wanasema bastola moja ya kimarekani,risasi 11, panga 7 na misokoto kadhaa ya bhangi zilipatikana kutoka kwa mshukiwa.

Mshukiwa anaaminika kuongoza kundi hilo kuwapora wakaazi na hata kuwajeruhi kwa kuwadunga kisu.

OCPD wa kisauni Richard Ngatia alisema polisi wanawasaka washukiwa wengine wanaoaminika kutoroka na akawataka wakazi kuwapa polisi habari zitakazowasaidia kuwanasa .

Kundi la wakali kwanza linaaminika kufadhiliwa na baadhi ya wanasiasa hapa mombasa na limekuwa likilaumiwa kwa visa vya kihalifu.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES