Mshindi Wa Gari Airtel Alenga Alama 430 Katika KCPE

Mshindi Wa Gari Airtel Alenga Alama 430 Katika KCPE

by -
0 548
Ranson Mbugua pamoja na mamake Agnes wakihojiwa studio Baraka FM

Hamu kubwa kwa Ranson Mbugua –mvulana wa umri wa miaka 14 ni kufaulu zaidi katika mtihani wa kitaifa K.C.P.E mwaka huu, na kuteuliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya kitaifa.

Mbugua Junior hata hivyo anaposubiri hilo mwishoni mwa mwaka, tayari ni mshindi wa kitaifa katika shindano la kibiashara la kampuni ya Airtel Kenya.

Mwanafunzi huyo wa darasa la 8 katika shule moja ya msingi wilayani Kisauni kaunti ya Mombasa alikabisdiwa gari jipya juma hili na wakurugenzi wa kampuni ya Airtel Kenya, kwa kuangukiwa na bahati nasibu.

“Kwa siku mbili mfululizo nikitoka shule nilikuta simu yangu imepigwa kwa namba nisiyoifahamu,baadaye nikaona namba yangu (kwa TV) na nikaambia wazazi wangu nipepigiwa simu kwamba nimeshinda gari lakini wakanipuuza wakisema hiyo namba ni ya matapeli”, Ranson Mbugua alisema katika mahijiano ya kipindi cha Bumburuka alipotembelea studio za Baraka FM Jumamosi asubuhi.

Alishinda gari aina ya Toyota Axio katika shindano la Smartika Na 5X Promotion ambapo kampuni ya Airtel Kenya inatoa magari 50 kwa muda wa siku 50.

Katika mahojiano na mtangazaji Neema Sulubu wa Baraka FM, Ranson alisema ndoto yake ni kupata alama 430 katika mtihani wa darasa la 8 –KCPE mwaka huu wa 2015 na kuteuliwa kujiunga na shule bora Kenya.

Alizuru Baraka FM pamoja na mamake mzazi Agnes wakiwa kwa gari hilo jipya lenye rangi nyekundu, likiendeshwa na babake mzazi bwana Mbugua.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES