Harambee Stars Yaadhibu Mauritius 5-2

Harambee Stars Yaadhibu Mauritius 5-2

by -
0 389
Harambee Stars players in celebration mood after scoring.

Kenya imepiga hatua katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Harambee Stars Jumanato jioni ilitandika Mauritius mabao 5-2 katika mechi iliyochezwa huko Mauritius.

Kufikia mapumziko Kenya iliongoza mabao mawili kwa bila yaliyofungwa na Johanna Omollo na Ayub Masika.

Makosa ya walinzi wa Harambee Stars yaliwezesha wenyeji Mauritius kupata mabao mawili licha ya Harun Shakava kufungia Kenya bao la tatu, na kufikia dadika ya sabiki mabao yalikuwa ni 3-2.

Lakini mabao mengine mawili kutoka kwa Johanna Omollo na Michael Olunga yalizidisha nguvu za Kenya, na hadi kipenga cha mwisho Harambee Stars ikashinda Mauritius mabao 5-2.

Mechi ya marudio itachezwa Nairobi Jumapili hii Oktoba tarehe 11 katika uwanja wa Kasarani, na iwapo Kenya itashinda imepangiwa kukutana na Cape Verde.

Baadaye shirikisho la soka barani Afrika –CAF litaorodheshwa timu zilizofuzu katika makundi na kucheza kuanzia mwaka wa 2016, kutafuta tiketi za kombe la dunia mwaka 2018.

Russia itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya FIFA ambayo Ujerumani ndio mabingwa watetezi kwa kushinda mwaka 2014 nchini Brazil.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES