Vyuo Vikuu Bora Duniani.

Vyuo Vikuu Bora Duniani.

by -
0 1464

Utafiti wa hivi punde uaonesha kuwa mataifa ya Marekani na Uingereza yana vyuo vikuu bora zaidi duniani.

Utafiti huo umeorodhesha Marekani kuwa na vyuo vikuu sita kati ya kumi bora kote dunini, huku Uingereza ikiwa na viwili na Switzerland chuo kimoja.

Chuo kikuu cha California Institute of Technology kimepewa nafasi ya kwanza ulimwenguni, kwa mujibu wa utafiti uliotolewa Jumatano Septemba 30 na shirika na PREMIUM TIMES WORLD UNIVERSITY RANKINGS.

California Institute of Technology imeshinda jumla ya vyuo vikuu 800 vilivyo-orodheshwa katika utafiti huo.

Nafasi ya pili ni chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza, nafasi ya tatu ni Stanford University Marekani, inafuata University of Cambridge Uingereza, na katika nafasi ya tano ni Massachusetts Institute of Technology nchini Marekani.

Kutoka bara la Afrika mna vyuo vikuu 13 kutoka nchi sita -Uganda, Nigeria, Ghana, Misri, Morocco na Afrika Kusini.

Hamna chuo kikuu chichote kutoka nchini Kenya katika orodha hiyo.

Makerere University ya Uganda imepata nafasi ya 401 miongoni mwa vyuo vikuu 800 bora duniani.

Nigeria –nchi iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika imetoa chuo kikuu kimoja tu katika orodha huyo, Ibadan University ambacho ni chuo cha zamani zaidi huko Nigeria.

University of Cape Town imechukua nafasi ya kwanza barani Afrika, huku ikiwa katika nafasi ya 120 kote duniani.

Shirika hilo la TIMES linasema ili kubaini vyuo vikuu bora lilichunguza vigezo vya kusomesha, utafiti, ubunifu, na jinsi chuo kinavyopokelewa katika ngazi ya kimataifa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES