David Beckham Dhidi Ya Zinedine Zidane

David Beckham Dhidi Ya Zinedine Zidane

by -
0 363
Kocha Sir Alex Ferguson

Kocha wa zamani aliyeongoza Manchester United kwa miaka 26 Sir Alex Ferguson, amealikwa kuongoza wachezaji katika mechi ya hisan.

Vyombo vya habari Uingereza vimeripoti kuwa kocha Ferguson ameungana tena na mchezaji wake wa zamani, na rafikiye –nyota David Beckham.

Mechi hiyo ya “Charity” itachezwa Novemba 14 uwanjani Old Trafford ambapo Sir Alex Ferguson atakuwa kocha wa kikosi cha wanasoka wakongwe wa England na Ireland.

David Beckham ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa Manchester United na timu ya taifa ya England, atakuwa kiranja wa kikosi hicho maalum cha “mastaa’ wastaafu.

Uingereza itacheza na kikosi maalum cha waliokowa wanasoka hodari duniani miaka ya nyuma, wakiongozwa na Zinedine Zidane wa Ufaransa.

Kocha wa timu hii ya “WORLD X1” atakuwa ni Carlo Ancelotti aliyewahi kuifunza Chelsea, Real Madrid na AC Milan.

Refarii wa mechi hiyo itakayochezwa Novemba 14 atakuwa ni Pierlluigi Collina kutoka Italy, ambaye mashabiki wanamfahamu zaidi kwa kunyolewa kipara.

Mechi hiyo ya kimataifa imevutia wafadhili wengi hasa kupitia matangazo ya kibiashara, na fedha itakayopatikana itasaidia kusaidia watoto kupitia shirika la UNICEF.

Comments

comments