Bunduki ya polisi wa upelelezi aliyeuawa yapatikana Majengo Mombasa

Bunduki ya polisi wa upelelezi aliyeuawa yapatikana Majengo Mombasa

by -
0 291

Polisi mjini Mombasa wamesema wamepata bunduki iliyokuwa ikitumiwa na afisa wa upelelzi aliyeuawa eneo la Old Town mjini humo mapema mwaka huu.

Bunduki hiyo iliwachwa na washukiwa wa ujambazi usiku wa kuamkia Ijumaa katika mtaa wa majengo Mombasa walipovamia duka moja eneo hilo kabla ya polisi kufika.

Washukiwa hao walimpiga risasi mhudumu wa duka hilo na kumjeruhi kichwani kabla ya kutoweka na kiasi cha fedha kisichojulikana na pia simu mbili.

Kamanda wa polisi eneo la pwani Francis Wanjohi amesema bunduki hiyo ni aina ya Ceska na imepatikana na risasi 14.

Wanjohi amedokeza kuwa washukiwa waliotoroka walikua watatu.

Aliyejeruhiwa anatibiwa katika hospitali ya Pandya mjini Mombasa.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES