Moses Kuria sasa kuhojiwa na ICC kuhusu matamshi yake

Moses Kuria sasa kuhojiwa na ICC kuhusu matamshi yake

by -
0 495

Mahakama ya kimataifa kuhusu Jinai -ICC inapanga kumhoji mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kufuatia matamshi yake kwamba alipanga mashahidi dhidi ya naibu rais William Ruto.

ICC imesema itakutana na Kuria tarehe 9 mwezi huu wa oktoba katika majengo ya bunge.

Majuma kadhaa yaliopita Kuria alidai kuwa yeye pamoja na aliyekuwa waziri wa haki Martha Karua walihusika kununua mashahidi dhidi ya Ruto.

Kulingana na gazeti moja ya humu nchini, ICC sasa inataka ufafanuzi zaidi kutoka kwa mbunge huyo kuhusu matamshi yake.

Ruto na Sang’ wanakabiliwa na mashtaka ya jinai kuhusu ghasia za uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya elfu moja waliripotiwa kuuawa.

Comments

comments