Shilingi milioni 40 zatengewa kilimo cha ufugaji kaunti ya Kilifi

Shilingi milioni 40 zatengewa kilimo cha ufugaji kaunti ya Kilifi

by -
0 536
Mfugaji akikama ng'ombe wa maziwa

Serikali ya kaunti ya Kilifi inasema imetenga shilingi millioni 40 mwaka huu wa kifedha kutekeleza miradi mbali mbali katika sekta kilimo.

Waziri wa kilimo kaunti ya Kilifi Mwalimu Menza alisema wananuia kuinua sekta ya kilimo kufuatia malalamiko kuwa sekta hiyo imewachwa nyuma kimaendeleo

Menza alisema fedha hiyo inalenga wakulima wa mifugo hasa wanaojihusisha na biashara ya kuuza maziwa.

Pia alidokeza kuwa serikali hiyo inaendeleza mpango wa kujenga vituo vya kukusanya maziwa katika maeneo ya Bamba na Marafa ili kuboresha sekta ya ufugaji mashinani.

Wakati huo huo alisema serikali hiyo imetia saini mkataba wa maelewano na wakfu wa benki ya KCB ambapo wakulima wafugaji wataruhusiwa kuchukua mikopo ya hadi shilingi milion 30.

Wakulima watalazimika kujiunga na vyama vya ushirika ili kufaidi mikopo hiyo na kunufaisha jamii ya kaunti hiyo.

Imehaririwa na Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES