Polisi wamuua mshukiwa wa wizi eneo la Nyali, Mombasa

Polisi wamuua mshukiwa wa wizi eneo la Nyali, Mombasa

by -
0 354

Maafisa wa polisi eneo la Nyali mjini Mombasa wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mshukiwa mmoja wa wizi.

Polisi hao wamedokeza kuwa mshukiwa huyo ameuawa walipofumaniwa wakitekeleza wizi katika nyumba moja ya kifahari eneo hilo la Nyali.

Pia wamearifu kuwa washukiwa walikuwa sita na wengine wamefanikiwa kutoroka na mali ya thamani kubwa.

Naibu afisa mkuu wa polisi huko Kisauni Walter Abonyo amesema wanawasaka washukiwa watano waliotoroka.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES