Mahakama yasimamisha mgomo wa walimu kwa siku 90.

Mahakama yasimamisha mgomo wa walimu kwa siku 90.

by -
0 417

Mahakama imesimamisha mgomo wa walimu kwa muda wa siku 90 ili kutoa nafasi ya majadiliano kati yao na serikali.

Pia imewaagiza walimu hao kurejea shuleni ifikiapo jumatatu wiki ijayo.

Wakati huo huo tume ya huduma za walimu TSC imeagizwa kuwalipa walimu hao wanaogoma mshahara wao wote wa mwezi huu wa septemba bila kukatwa.

Walimu waligoma kutaka serikali itimize agizo la mahakama la kuwapa nyongeza ya mshahara ya kati ya asilimia 50-60.

Mgomo huo wa walimu umeendelea kwa wiki ya 3 huku serikali ikilazimika kufunga shule zote za umma.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES