Cord yasistiza kuunga mkono mgomo wa Walimu.

Cord yasistiza kuunga mkono mgomo wa Walimu.

by -
0 353

Muungano wa kisiasa wa CORD umesisitiza  kuwa utaendelea kuunga mkono mgomo wa walimu hadi pale serikali itakapowalipa nyongeza ya mishahara yao..

Viongozi wa CORD wakiwemo Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula walisisitiza hayo kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa jumatano katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi.

Hayo yanajiri huku ikibainika kwamba walimu watasusia kusimamia mitihani ya kitaifa KCPE na KCSE huku watahiniwa wa kidato cha nne wakitarajiwa kuanza mtihani wiki ijayo.

Vyama vya walimu KNUT na KUPPET vimeagiza walimu kususia zoezi hilo hadi mahitaji yao yatimizwe.

Walimu waligoma kushinikiza nyongeza ya mishahara ya aslimia 50-60 kama ilivyoamuliwa na mahakama ya juu zaidi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES