Uhaba wa maji watatiza Kilifi.

Uhaba wa maji watatiza Kilifi.

by -
0 561

Uhaba wa maji unaoshuhudiwa kaunti ya kilifi umeathiri pakubwa huduma katika mikahawa mingi mjini Kilifi.

Tatizo hilo limekuwa kwa zaidi ya majuma mawili sasa.

Wafanyabiashara katika mikahawa wamesema biashara zao zimeathirika pakubwa huku wakihofia kufungwa kwa hoteli nyingi.

Wanalaumu kampuni ya huduma za maji eneo hilo ya Kimawasco kwa masaibu hayo.

Hata hivyo mkurungenzi mkuu wa kampuni hiyo mhandisi Makupe Mwamuye, amesema wanashughulikia tatizo hilo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES