#Usain Bolt Akiri Ugumu Mbioni

#Usain Bolt Akiri Ugumu Mbioni

by -
0 384
Usain Bolt akishinda dhahabu katika mbio za mita 100.

Usain Bolt wa Jamaica amekiri kuwa ushindi wake katika mbio za mita 100 huko Beijing nchini Uchina, haukuwa rahisi.

Bolt anasema hili lilikuwa shindano lake ngumu zaidi maishani na kamwe hatalisahau.

“Niling’ang’ana sana kumshinda Justin Gatlin pamoja na wengine waliokwa katika fainali hapa Beijing,” alisema Bolt ambaye tangu mwaka 2014 alisumbuliwa na jeraha.

Mwanariadha huyo wa Jamaica alikimbia kwa muda wa sekunde 9.79 kushindia nchi yake nishani ya dhahabu.

Bolt pia ndiye bingwa wa Olympiki katika mbio za mita 100 na 200, akishikilia rekodi za dunia –sekunde 9.58 na sekunde 19.19 mtawalia.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES