Greg wa Uingereza Ashinda Long Jump

Greg wa Uingereza Ashinda Long Jump

by -
0 433
Rekodi ya dunia ya Long Jump ni mita 8.90.

Greg Rutherford kutoka Uingereza sasa ndiye bingwa wa dunia katika shindano la kuchupa umbali, yaani Long Jump.

Rutherford ambaye pia ni bingwa wa Olympiki Jumanne mchana alishinda nishani ya dhahabu mjini Beijing, China, kwa kuchupa umbali wa mita 8.41.

Rekodi ya dunia ya Long Jump ni mita 8.90 iliyowekwa katika michezo ya Olympiki mwaka wa 1968 huko Mexico City, na mwanamichezo Bob Beamon.

Mtu wa kwanza kuruka mita 8.13 alikua ni Jesse Owens –mwanariadha hodari wa Marekani mwaka wa 1935.

Nchini Kenya rekodi ya Long Jump ni mita 8.12 iliyowekwa Septemba 14 mwaka wa 1995 na Jacob Katonon, mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES