#EzekielKemboi Ampenda Sonko,Ida Odinga

#EzekielKemboi Ampenda Sonko,Ida Odinga

by -
0 434
Ezekiel Kemboi -bingwa mara 4 wa dunia.

Ezekiel Kemboi –bingwa mara nne (mfululizo) wa dunia katika mbio za mita 3,000m kuruka vizuizi na maji alikiri Jumatatu urafiki wake na seneta wa Nairobi Mike Mbuvi, maarufu Sonko.

Kemboi ambaye sasa umri wake ni miaka 33 alidokeza hilo akiwa mjini Beijing,China,muda mfupi baada ya kunyakua nishani ya dhahabu katika fainali ya kuruka vizuizi na maji (3,000m SteepleChase).

“Rafiki yangu Sonko alinipigia simu jana kunipa motisha ili nishindie nchi yetu dhahabu tena,’ Kemboi aliwaambia waandishi wa habari za michezo huku akisherehekea dhahabu yake ya nne mfululizo, katika mbo za dunia zinazoandaliwa na shirikisho la IAAF kila baada ya maika miwili.

Aliongeza kuwa ushindi huo anautoa kwa watu watatu anaowaenzi nchini Kenya: Mwanamuziki Jaguar ambaye jina lake halisi ni Charles Kanyi, Mike Mbuvi Sonko, na bi Ida Betty Odinga -mke wa kinara wa muungano wa CORD Raila Odinga.

Kando na kushinda nishani ya dhahabu katika michezo ya Olympiki mwaka wa 2004 mjini Athens,Ugiriki, Ezekiel Kemboi amefanikiwa kushinda dhahabu za ubingwa wa dunia mara nne mfululizo; 2009 mjini Berlin-Ujerumani, 2011 mjini Daegu-Korea Kusini, 2013 mjini Moscow-Russia, na sasa 2015 makala ya 15 huko Beijing, Uchina.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES