Vijana Wamnusuru Mwanamke Mshukiwa Wa Dawa Za Kulevya

Vijana Wamnusuru Mwanamke Mshukiwa Wa Dawa Za Kulevya

by -
0 356

Vijana waliokuwa wamejihami kwa visu na panga wamevamia kituo kimoja cha mabasi hapa mjini Mombasa na kumwokoa mwanamke aliyezuiliwa kwa kushukiwa kusafirisha dawa za kulevya.

Mwanamke huyo alizuiwa na wahudumu wa kituo hicho cha mabasi kilicho eneo la Bondeni.

Wahudumu wa kituo hicho wanasema vijana hao walifika ghafla na kuwaagiza kumwachilia mshukiwa huku wakitishia kuwashambulia.

Walimnusuru mwanamke huyo na kutoroka naye.

Comments

comments