Meli Kubwa Zaidi Yatia Nanga Bandarini Mombasa

Meli Kubwa Zaidi Yatia Nanga Bandarini Mombasa

by -
0 754
Meli kwa jina Clemens Schulte -Kubwa zaidi kuwahi kutia nanga katika bandari ya Kilindini Mombasa

Meli kubwa zaidi kwa uwezo wa kubeba uzani na pia upana wake, imetia nanga bandarini Mombasa.

Meli hiyo kwa jina Clemens-Schulte ilitia nanga Jumanne usiku.

Ina uwezo wa kusheheni shehena takriban elfu 6 na ni ya kwanza kama hiyo kuwahi kutua bandarini Mombasa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari ya Mombasa Gichiri Ndua anasema uzinduzi wa Gatti ya 19 umevutia meli kubwa zaidi hivyo kupanua huduma za bandarini.

Ndua amesema wanalenga kuzindua sehemu nyingine ya kuhifadhi shehena kufikia mwezi Machi mwakani.

Amedokeza kuwa sehemu hiyo itakua na uwezo wa kuhifadhi shehena zaidi ya elfu 500.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES