#Mwanasiasa Seb Coe Amshinda Mwalimu Sergey Katika Urais IAAF

#Mwanasiasa Seb Coe Amshinda Mwalimu Sergey Katika Urais IAAF

by -
0 374
Sebastian Coe (Uingereza) na Sergey Bubka (Ukraine) wagombea pekee urais wa IAAF.

Bingwa wa zamani wa Olympiki Lord Sebastian Coe wa Uingereza sasa ndiye rais mpya wa shirikisho la kimataifa la riadha –IAAF.

Seb Coe aliyeshinda dhahabu katika mbio za mita 1500 mwaka wa 1980 mjini Moscow na pia mwaka 1984 mjini Los Angeles, alishinda kiti cha urais katika uchaguzi wa IAAF uliofanyika mapema Jumatano.

Alishinda kwa kura 115 dhidi ya kura 92 za mpinzake wa pekee Sergey Bubka wa Ukraine –aliyeshikilia rekodi ya dunia kwa miaka mingi kuruka Pole Vault mita 6.15.

Tofauti kati ya wanariadha hao wawili wastaafu ni kuwa Seb Coe aliye na umri wa miaka 58 alijiunga na ulingo wa siasa na kuwa mbunge kwao Uingereza, lakini mwenzake Sergey Bubka mwenye umri wa miaka 51 aliendeleza masomo ya juu kuhusu sayansi ya viungo vya mwili, akiwa mwalimu wa michezo (P.E),

Lord Sebastian Coe sasa ni rais wa sita wa shirikiaho la IAAF ambalo lilizinduliwa miaka 103 iliyopita.

Amemrithi rais Lamine Diack wa Senegal ambaye anastaafu rasmi Agosti tarehe 31, siku moja baada ya kukamilika mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia mjini Beijing, Uchina.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES