#Isaiah Kiplagat Aambulia Patupu IAAF

#Isaiah Kiplagat Aambulia Patupu IAAF

by -
0 772
Isaiah Kiplagat ameongoza chama cha riadha Kenya KAAA/AK tangu mwaka wa 1992

Rais wa chama cha riadha nchini Kenya Isaiah Kiplagat mapema Jumatano alikosa kuchaguliwa, katika uchaguzi wa shirikisho la kimataifa la riadha -IAAF uliofanyika mjini Beijing, Uchina.

Kiplagat aliyefanya kampeni kwa miezi mitatu akiwa ameacha hatamu za uongozi wa AK kwa maafisa wenzake Kenya, alikuwa akigombea wadhifa wa naibu-rais wa shirikisho hilo la kimataifa.

Licha ya yeye mwenyewe kusafiri hadi mjini Beijing alikokosa kuchaguliwa, atasalia kuwa mwanachama wa baraza kuu la IAAF, aliloteuliwa tangu mwaka wa 1999.

Sasa manaibu wapya wa rais waliochaguliwa (kawaida huwa 4) ni Dahlan al-Hamad wa Qatar, Hamad Kalkaba Malboum wa Cameroon, Alberto Juantorena wa Cuba, na Sergey Bubka wa Ukraine.

Katika uchaguzi wa manaibu-rais wa IAAF aliyeongoza ni Sergey Bubka kwa kura 187, Dahlan kura 159, Kalkaba kura 115 na Juantorena aliyepata kura 111.

Isaiah Kiplagat alikuwa wa mwisho kwa kupata kura 64, baada ya mwafrika kwenzake Hamad Kalkaba wa Cameroon kukataa kumpisha.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES