Washukiwa Wa Uwindaji Haramu Wakamatwa Kilifi

Washukiwa Wa Uwindaji Haramu Wakamatwa Kilifi

by -
0 355

Polisi kaunti ya Kilifi wanawazuilia washukiwa wawili wa uwindaji haramu wanaodaiwa kupatikana na ngozi za Wanyama pori.

Washukiwa hao wanadaiwa kupatikana na ngozi tatu za Chui na mbili za mnyama Duma.

Polisi wanasema waliwawekea mtego washukiwa hao ambao ni wakaazi wa Ganze, Kaunti ya Kilifi, kwa kuwadanganya kuwa wangenunua ngozi hizo endapo wangewasafirishia hadi mjini Kilifi.

Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye Jumanne na endapo watapatikana na makosa basi wanaweza kutozwa faini ya hadi shilingi millioni 20 au kutumikia kifungo cha hadi miaka mitano.

Imehaririwa na E. Mwachoni

Comments

comments