#Simba Mlafi Apelekwa Hospitali

#Simba Mlafi Apelekwa Hospitali

by -
0 759

Simba ambaye amekuwa akihangaisha mifugo katika kaunti ya Tana River alikamatwa na kupelekwa hospitali!

Madaktari wa mifugo walilazimika kumkagua samba huyo ili kubaini iwapo yuko timamu kiafya, kabla ya kuhamishwa hadi Mbuga ya wanyama ya Tsavo East.

Alikamatwa na kusafirishwa na maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama-pori KWS eneo la Tana River, wakiongozwa na afisa mkuu Mathias Mwavita.

Wenyeji wa kijiji cha Gafuru walitaka Simba huyo afungiwe katika kituo cha Polisi, kwa kuendelea kuhangaisha Ng’ombe wao!

Comments

comments