Shirika la CNN laomba wakenya msamaha

Shirika la CNN laomba wakenya msamaha

by -
0 372

Shirika la habari la CNN hatimaye limeomba Kenya msamaha kuhusiana na taarifa iliyotaja nchi hii kama kitovu cha ugaidi.

Naibu rais wa CNN Tony Maddox, alhamisi aliwasilishwa rasmi msamaha kwa wakenya kupitia rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi.

Maddox alisema CNN ilisikitishwa na hisia za wakenya baada ya taarifa hiyo na kwamba inatambua juhudi za taifa hili hasa katika kupambana na ugaidi.

CNN ilitoa matamshi hayo wakati rais wa Marekani Barack Obama akitarajiwa kuwasili nchini, jambo lililozua hamaki miongoni mwa wakenya.

Wakenya wa tabaka mbalimbali walikasirishwa na taarifa hizo na kuonyesha ghadhabu zao kupitia mitandao ya facebook na Twitter wakitaka CNN iseme ukweli na kuomba radhi kwa taarifa hizo za uwongo na kupotosha.

Katika mazungumzo yake na mkuu huyo, rais Kenyatta alisema nia ya Kenya sio kuficha maovu au changamoto zake, lakini akaitaka CNN kusema ukweli wa mambo jinsi yalivyo badala ya kuchapisha au kutangaza taarifa zisizokuwa na msingi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES