Mashua ya mihadarati yalipuliwa baharini

Mashua ya mihadarati yalipuliwa baharini

by -
0 461

Mashua iliyonaswa ikiwa imebeba mihadarati ya kilo 7.6 yenye thamani ya shilingi milioni 20 imeharibiwa pamoja na dawa hizo.

Mashua hiyo kwa jina baby Iris, ilikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi tangu ikamatwe na sasa imelipuliwa katika bahari hindi.

Shughuli hiyo ilianza na upimiaji uzani wa dawa hizo aina ya Heroine iliyofanyika katika maabara ya bandari ya Mombasa.

Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery alihudhuria hafla hiyo.

Maafisa wa jeshi wamehusika na ulipuaji huo kwa kutega vilipuzi ndani ya mashua hiyo kabla ya kuiharibu kabisa.

Mwaka jana rais Uhuru Kenyatta aliongoza jeshi la KDF katika shughuli ya kulipua meli iliyokamatwa na dawa za kulevya.

RaIS alisema mbinu hiyo mpya itasaidia katika vita dhidi ya mihadarati.

Comments

comments