Wanafunzi Wafa Maji Diani Ukunda.

Wanafunzi Wafa Maji Diani Ukunda.

by -
0 564

Wanafunzi 7 wa shule ya msingi ya St Martin huko Murang’a wamethibitishwa kufa maji baharini huko Diani kaunti ya Kwale.

Imearifiwa kuwa walizama baada ya kulemewa na mawimbi mazito walipokua wakiogelea wakiwa na wenzao mwendo wa saa kumi na mbili unusu jumatano jioni.

Duru zinasema kwamba kufikia sasa ni miili 3 pekee iliyopatikana huku hali mbaya ya anga ikiathiri shughuli za uokoaji.

Wanafunzi hao walikuwa wakiogoelea baharini bila uangalizi wa wapiga mbizi.

Kamishna wa kaunti ya Kwale Evans Achoki amesema shughuli za uokoaji zingali zinaendelea.

Visa vya watu kufa maji hapa pwani vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara hususan wanaotoka sehemu zingine za nchi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES