Walimu 800 Waondolewa Kaskazini Mashariki .

Walimu 800 Waondolewa Kaskazini Mashariki .

by -
0 339

Tume ya huduma za walimu TSC hatimaye imewapa uhamisho walimu 886 kutoka kaskazini Mashariki,baada ya walimu hao kuapa kwamba hawatorudi sehemu hizo kutokana na ukosefu wa usalama.

Walimu hao walitarajiwa kuanza kazi rasmi leo katika maeneo tofauti kama vile hapa Mombasa,Kilifi,Turkana, na Lamu baada ya kesi iliyokuwa kortini kuhusu hatma yao.

Lakini hatma ya walimu wengine 200 wanaofunza sehemu hizo za Kaskazini Mashariki bado haijulikani.

Chama cha walimu KNUT kimedhibitisha habari hizo za uhamisho wa walimu hao kwasababu za kiusalama.

Jumla ya walimu 20 waliuawa na magaidi Mandera kisha baadae watu 148 wakauwa na magaidi sehemu hiyo hiyo wengi wao wakiwa wanafunzi.

Comments

comments