Upimaji Mashamba Ya Waitiki Kuanza Jumanne.

Upimaji Mashamba Ya Waitiki Kuanza Jumanne.

by -
0 381

Zoezi la kupima mashamba ya Waitiki eneo la Likoni hapa Mombasa, litaanza jumanne ya tarehe 11.

Maafisa 25 kutoka jijini Nairobi wako hapa Mombasa tayari kwa shughuli hiyo.

Zoezi hilo linajumuisha kuchukua majina ya wakazi wanaoishi katika shamba hilo na linatarajiwa kuchukua siku 10.

Shamaba hilo la Waitiki limekuwa likikumbwa na mzozo kuhusu umiliki.

Wakazi wanaoishi ardhi hiyo wamesemekana kuwa na wasiwasi wa kufurushwa, lakini serikali ikaahidi kumlipa fidia mwenye ardhi hiyo kwa jina Waitiki, ili wasifurushwe.

Comments

comments