Mabaharia Wakenya Wakwama Karibu Na Somalia.

Mabaharia Wakenya Wakwama Karibu Na Somalia.

by -
0 331

Mabaharia 14 wa Kenya wamekwama katika maji makuu ya bahari Hindi karibu na jimbo la Puntland nchini Somalia.

Kulingana na afisa wa ubaharia Andrew Mwangura, wengi wa mabaharia hao wanatoka eneo la Likoni hapa Mombasa.

Mwangura anasema mabahari hao wamekwama baharini kwa muda mrefu baada ya mashua yao kukumbwa na hitilafu za kimitambo.

Mabahari hao miongoni mwao raia kadhaa wa kigeni, walikuwa katika maji makuu kwa shughuli za uvuvi.

Eneo hilo pia linasemekana kuwa ngome ya maharamia ambao katika miaka ya hivi karibuni, walikuwa kero katika maji hayo makuu hasa ghuba ya Aden.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES