#Mkasa Wa Boti Waua Watu 200 Baharini Mediterranean

#Mkasa Wa Boti Waua Watu 200 Baharini Mediterranean

by -
0 541

Watu zaidi ya 200 wanahofiwa kufa-maji katika bahari ya Mediterranean, ambako mashua ilizama mapema Alhamisi ikiwa na abiria zaidi ya 600.

Mashua hiyo ilizama karibu na pwani ya Libya muda mfupi baada ya kupata matatizo ya usafiri baharini.

Mashirika zaidi ya 10 yamekuwa yakiendelea na shughuli za uokoaji.

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka –MSF ni miongoni mwa makundi ya waokoaji yaliyozuru eneo la mkasa.

Wahudumu wa shirika hilo wanasema japo shughuli ya uokoaji ni ngumu, wamefaulu kuwanusuru watu wengi.

Inaaminika mashua hiyo iliyotengenezwa kwa mbao, ilikuwa ikibeba hadi watu 600 au zaidi.

Inaaminika kufikia Alhamisi mchana watu wapatao 300 walikuwa wamenusurika kwa kuokolewa.

Juan Matias –mmoja wa wahudumu wa shirika la MSF, anasema hali waliyoshuhudia baharini ni ya kuogofya.

Meli zaidi zimewasili eneo la ‘Mediterranian Sea’ kuwasaidia katika uokoaji.

Majeruhi wengine wamesafirishwa kwa ndege aina ya helicopter, kutafutiwa matibabu zaidi.

Takwimu zinaonesha kuwa watu zaidi ya 2,000 wamefariki katika miaka ya hivi karibuni, wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kuingia Ulaya.

Wengi ni wahamiaji kutoka barani Afrika.

Comments

comments