#FIFA Yatangaza Timu Bora

#FIFA Yatangaza Timu Bora

by -
0 386

Shirikisho la soka duniani –FIFA Alhamisi asubuhi lilitoa orodha mpya ya timu za taifa, kulingana na ubora wa viwango vya mpira wa miguu.

Harambee Stars ya Kenya imesalia pale pale ilipokuwa Julai mwaka huu, katika nafasi ya 116 kote dunaini.

Barani Afrika Kenya imeorodheshswa katika nafasi ya 35, ikiwa imefikisha alama 266.

Uganda Cranes inaendelea kuongoza eneo la Afrika mashariki na kati (CeCaFa), ambapo kwa sasa inashikilia nafasi ya 74, yaani pointi moja nyuma ya Zambia.

Algeria bado ndio timu bora barani Afrika ikiwa na alama 19, na jumla ya alama 941.

Timu za Afrika zinazofuata ni Ivory Coast, Black Stars ya Ghana, Tunisia, na Senegal nafasi ya tano.

FIFA imeorodhesha Argentina kama timu bora duniani, ikisalia kileleni kwa kuzoa alama 1425.

Ubelgiji inashikilia nafasi ya pili, Ujerumani ya tatu, Colombia nafasi ya nne, na Brazil ikifunga orodha ya tano bora.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES