Wahanga Wa Ghasia Za Uchaguzi Bado Wamwandama Rais Uhuru.

Wahanga Wa Ghasia Za Uchaguzi Bado Wamwandama Rais Uhuru.

by -
0 430

Wahanga wa ghasia za uchaguzi wa mwaka 2007 sasa wanataka mahakama ya ICC iagize uchunguzi mpya dhidi ya rais Uhuru Kenyatta.

Kupitia wakili wao – Fergal Gaynor, wahanga hao walisem upande wa mashtaka ulifanya uchunguzi duni ambao.

Walisema uchunguzi dhabiti ungehakikisha rais Kenyatta na washukiwa wengine wakati huo Meja-Generali Hussein Ali na Francis Muthaura wanahukumiwa.

Aidha wanataka mwendesha mashtaka Fatou Bensuda aagizwe kutoa nakala za ushahidi wa kesi ili kueleze namna alivyojipanga kwa kesi hizo.

Madai dhidi ya rais Kenyatta, Muthaura na Ali yalisambaratika kabla ya kufika hatua ya kesi kuanza rasmi.

Ghasia hizo za mwaka 2007, zilisababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja huku wengine nusu milioni wakitoroka makwao.

Comments

comments