Mdahalao Kuhusu Chama Cha Kisiasa Pwani.

Mdahalao Kuhusu Chama Cha Kisiasa Pwani.

by -
0 352

Mdahalo mkali unaendelea nchini na hata pwani kwa jumla kuhusu azma ya muungano wa jumuiya ya kaunti za pwani.

Kiongozi wa hivi punde kutilia shaka lengo la jumuiya hiyo ni mbunge wa Voi Jones Mlolwa.

Alisema hana uhakika iwapo lengo la muungano huo ni kuinuia uchumi wa kaunti za pwani.

Naye mbunge wa Wundanyi Thomas Mwadeghu alisema badala ya kutumia Jumuiya kimaendeleo, viongozi wanatumia kujiimarisha kisiasa mwaka wa 2017.

Tangu muungano huo ubuniwe, kumekuwa na hali ya sitofahamu kuhusu ajenda zake huku baadhi ya wabunge wakidai kuwa hiyo ni njama ya magavana wa pwani kutumia muungano huo kujipigia debe ili kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2017.

Comments

comments