#Namibia Yashinda Msumbiji 2-0 Fainali ya COSAFA

#Namibia Yashinda Msumbiji 2-0 Fainali ya COSAFA

by -
0 643

Namibia imeshinda kombe la COSAFA baina ya mataifa ya kusini mwa bara la Afrika, kwa mara ya kwanza katika historia.

Timu ya taifa ya Namibia maarufu kama “Brave Warriors” ilifunga Msumbiji mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa Jumamosi jioni nchini Afrika Kusini.

Mshambuliaji matata Deon Hotto alifunga mabao yote mawili na kuibuka miongoni mwa wachezaji waliofunga mabao mengi, na manne katika makala ya mwaka huu ya COSAFA.

Kocha wake Ricardo Monnetti pia alisisimua mashabiki wakati wote wa mashindano hayo,na kusaidia nchi yake kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.

Ushindi wa Namibia ni onyo kwa timu ya Kenya –Harambee Stars ambao wamepangwa kundi moja, katika mechi za kufuzu kwa dimba la kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao wa 2016.

Katika mechi za nusu-fainali Namibia ilifunga Madagascar mabao 3-2 wakati Mozambique ikilaza Botswana mabao 2-1 na kufuzu kwa fainali.

Timu 14 zilishiriki michuano ya mwaka huu ya COSAFA iliyoandaliwa nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars ya Tanzania pamoja na Black Stars ya Ghana zilishirikishwa kama time geni, ambazo sio wanachama wa shirika la COSAFA.

Comments

comments