Mtu Amdunga Kisu Mkewe Kisha Akajiua.

Mtu Amdunga Kisu Mkewe Kisha Akajiua.

by -
0 429

Mwanamume wa umri wa miaka 37 katika lokesheni ya Kishushe eneo bunge la Wundanyi kaunti ya Taita Taveta amemjeruhi mkewe kwa kumdunga kisu na kisha akajitoa uhai.

Imearifiwa kuwa tukio hilo huenda lilichangiwa na mzozo wa kinyumbani.

Jina la marehemu limetolewa kama William Mwamburi .

Kamanda wa polisi kaunti ya Taita Taveta Richard Bitonga anahimiza wakaazi katika kaunti hiyo kutumia njia muafaka kutatua matatizo katika jamii.

Wakati huo huo mwanaume wa umri wa miaka 20 katika eneo la Teita Sisal eneo bunge la Mwatate katika kaunti hiyo ameripotiwa kujitoa uhai baada ya kukatazwa na nduguye dhidi ya kujihusisha kimapenzi na mwanamke wa umri wa miaka 50.

Miili yao inahifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi

Comments

comments