Gavana Joho Akosoa Wabunge Kwasababu Ya Picha .

Gavana Joho Akosoa Wabunge Kwasababu Ya Picha .

by -
0 505

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ameonekana kukosoa hatua ya wabunge wa kaunti kupitisha hoja ya kutaka sehemu zote za biashara Mombasa kutundika picha yake.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Gavana Joho badala yake amewashauri wabunge hao kujadili mambo muhimu ambayo ni ya manufaa kwa wananchi.

Hii ni baada ya bunge hilo kupitia mswada uliowasilishwa bungeni humo, kuwataka wafanyabiashara wote katika kaunti hii kubandika picha ya Joho katika sehemu zao kama heshima.

Kupitia taarifa hiyo, Joho anaashiria kuukataa mswada huo utakapowasilishwa kwake kuuweka sahihi ya kuwa sheria.

Comments

comments