Walemavu Kilifi Wapewa Ufadhili Wa Mamilioni Ya Pesa.

Walemavu Kilifi Wapewa Ufadhili Wa Mamilioni Ya Pesa.

by -
0 385

Walemavu katika kaunti ya Kilifi, wamepokea vifaa vya thamani ya shilingi milioni 1.8 kutoka serikali ya Kitaifa.

Wakiongozwa na msimamizi wa masuala ya ulemavu kaunti hiyo Nyasaida Famau, walisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi wakidai kusahaulika na kuitaka serikali ya Kitaifa na ile ya kaunti kujenga vituo zaidi vya walemavu kusomea.

Kulingana na msimamizi wa miradi ya walemavu katika wizara ya vijana, michezo na walemavu katika serikali ya kitaifa Bernard Adowe, vifaa hivyo vimetokona na mgao wa shilingi milioni 6 zilizotengewa mkoa wa pwani kati ya shilingi milioni 100 iliyotengewa walemavu nchini.

Vifaa hivyo ni pamoja na Cherehani, baiskeli na majembe ya ng’ombe kwa ajili ya shughuli za ukulima.

Comments

comments