Mtaa Wa Old Town Hapa Mombasa Wainyima Serikali Kuu Usingizi.

Mtaa Wa Old Town Hapa Mombasa Wainyima Serikali Kuu Usingizi.

by -
0 376

Serikali sasa imesema inatafakari mbinu itakayotumia kurejesha hali ya usalama katika mji wa old town hapa Mombasa ambao umeonekana kudorora kiusalama siku za hivi karibuni.

Hii ni kufuatia misururu ya visa vya uhalifu vikiwemo uporaji wa mali na hata majeruhi kwa wanaokaidi majambazi hao.

Naibu kamishna wa kaunti ya Mombasa- Salim Mahamoud aliongoza mkutano wa dharura uliojumuisha machifu na wazee wa mitaa lengo likiwa kusafisha sifa ya mtaa huo.

Mahamoud aidokeza kuwa majambazi wanaohangaisha mtaani huo wana umri mdogo lakini serikali sasa haitosita kuwakabili.

Comments

comments