Mashirika Ya Haki Afrika Na Muhuri Yatafakari Kufungiwa Nje

Mashirika Ya Haki Afrika Na Muhuri Yatafakari Kufungiwa Nje

by -
0 438

Viongozi wa mashirika ya kijamii hapa Mombasa wanasema wataenda mahakamani ikiwa watathibitisha madai ya kufutiliwa mbali kwa leseni zao za kuhudumu.

Mwenyekiti wa shirika la kiisalmu la MUHURI Khelif Khalifa aliambia Baraka Fm kwamba wamekuwa wakihudumu kisheria tangu mwaka 1997, na habari kwamba leseni ya shirika lao imefutiliwa mbali zimewashangaza.

Khalifa alisema iwapo habari hizo ni kweli, huenda hatua hiyo imechangiwa kisiasa kutokana na harakati zao za kutetea haki.

Lakini mkurugenzi wa Muhuri Hassan Abdhile alitatiza mahojiano baina ya wanahabari na mwenyekiti wa shirika hilo na kuwafukuza akidai wanachapisha habari za kupotosha.

Nalo shirika la Haki Afrika lilisema halijapokea taarifa zozote rasmi kuhusiana na kufutiliwa mabali kwa leseni yao.

Wanasema walipata taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari.

Serikali ilidai mashirika hayo mawili yanafadhili ugaidi nchini, na hivi maajuzi ilifunga akaunti za benki za mashirika hayo.

Mashirika hayo yaliwasilisha kesi mahakamani kutaka akaunti hizo zifunguliwe, na kesi hiyo inaendelea mahakamani.

Comments

comments