Mahakama Mombasa Yamnyima Dhamana Mshukiwa Wa Ugaidi.

Mahakama Mombasa Yamnyima Dhamana Mshukiwa Wa Ugaidi.

by -
0 439

Mahakama ya Mombasa imemnyima dhamana mshukiwa wa ugaidi aliyekamatwa mapema wiki hii katika eneo la Bondeni,Mombasa.

Hakimu wa mahakama hiyo Richard Odenyo, pia aliipa idara ya polisi siku 30 kukamilisha uchunguzi wao kuhusiana na kesi hiyo.

Odenyo alisema hakuona sababu ya kunyima upande wa mashtaka muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wao kama ulivyowasilisha ombi kwake.

Mshukiwa huyo Sheikh Khalid Mohamed, alidaiwa kumiliki vilipuzi pamoja na kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Al shabab lenye ngome yake nchini Somalia.

Lakini Wakili wake Jeff Asige, alidokeza kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Comments

comments