OCS Wa Watamu Ashambuliwa Na Raia.

OCS Wa Watamu Ashambuliwa Na Raia.

by -
0 471

Afisa mkuu wa polisi wa kituo cha Watamu kaunti ya Kilifi, ameshambuliwa na kujeruhiwa na umati wa watu.

Duru zinasema kuwa OCS Michael Ngonga alipigwa mawe na wakazi waliojawa na ghadhabu, baada ya afisa huyo kumwokoa mshukiwa aliyedaiwa kumdunga mtu kisu.

Wananchi hao walitaka kumshambulia mshukiwa huyo lakini maafisa wa polisi wakamwokoa ambapo raia walimaliza hasira zao kwa OCS huyo.

Gari la polisi la kituo hicho pia liliharibiwa kwenye kisa hicho,kwa kupurwa mawe,wakati maafisa wa polisi wakimwokoa mshukiwa huyo na kumwingiza ndani ya gari.

Mkazi mmoja aliyeshuhudia alisema OCS huyo alikuwa akivuja damu usoni baada ya kupigwa mawe akijaribu kuingia ndani ya gari la polisi.

Comments

comments