Muhuri Na Haki Afrika Zapokonywa Leseni Za Kuhudumu.

Muhuri Na Haki Afrika Zapokonywa Leseni Za Kuhudumu.

by -
0 511

Bodi ya kusimamia mashirika yasiyo ya serikali, imefutilia mbali leseni za kuhudumu za mashirika ya kutetea haki za binadamu ya MUHURI na HAKI AFRIKA hapa Mombasa.

Serikali ilifunga akaunti za benki za MUHURI na Haki Afrika baada ya kudai kwamba mashirika hayo yalikuwa yanafadhili shughuli za ugaidi nchini.

Taarifa ya bodi hiyo imetolewa kupitia mitandao ya kijamii nchini.

Kulingana na afisa wa MUHURI Fahad Changi,bado hawajapokea taarifa rasmi kutoka kwa bodi hiyo kuhusu hatua hiyo,lakini alisema itabidi mashirika hayo kuwasilisha kesi kortini kupinga kauli hiyo.

Mashirika hayo yaliwasilisha kesi kortini kupinga hatua ya serikali kufunga akaunti zao.

Comments

comments